Social Icons

Featured Posts

Friday, November 22, 2013

KAMATI KUU YA CHADEMA YAWAVUA UONGOZI ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO NA SAMSONI MWIGAMBA

Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande. Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu kulichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejukana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema. Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2. Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA. Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu 
Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.

Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.

Wednesday, January 2, 2013

NMB MAKETE YAMWAGA ZAWADI KWA WAGONJWA

Katika kusherekea sikuu ya mwakampya benki ya NMb tawi la Makete  ilitembea katika hospitali ya wilaya ya Makete na kuwaliwaza wagonjwa pamoja na kuwapa zawadi za mwaka mpya .
 
Meneja wa benki hiyo bwana Anyambilile Ambingile alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuona niviziri wakaenda kuwaona wagonjwa ambao wapo katika hospitali hiyo ili kuwapa moyo wangonjwa pamoja na kuwapa zawadi za mwaka mpya jambo ambalo litawafanya waongeze matumaini kuweza kupona na baadaye kiruhusiwa kutoka na wao kama taasisi kuwapa faraja 
 
Adha Ambingile aliyaomba mashirika taasisi  za dini pamoja serikali kuiga mfano huo kwa kuwatembelea mara kwa mara watu kama hao kwani kwa kufanya hivyo kunaleta mahusiano mazuri kati ya jamii na taasisi “tunaomba jamii ielewe kuwa suala la kuwasaidi watu katika jamii ni la kila mtu aliyenacho ndo maana nasema mashika yaige mfano huu ilikujijengea mazingira mazuri na ushikiano mzura baina ya taasisi na jamii kwani kwa kufanya hivyo kutasadia jamii iwe na mtazamo mzuri na kwa taasisi hizo”alisema Ambingile
 
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa wilaya Michael Guraka alipongeza kitendo hicho na kuwapongeza benki hiyo kwa kuwakumbuka wagonjwa hao ambao wamekuwa wakikosa furaha hasa katika msimu huu wa sikuu kwani huwa wanakosa liwazo kwaupande wake Rehema Mahenge ambaye alilazwa katika wodi ya wazazi alishukuru kwa uongozi mzima wa benki hiyo kwa kuwakumbuka wagonjwa na kuwaomba kundlea kufanya hayo zaidi katika siku za usoni na wasishi hapo

Monday, December 17, 2012

MBUNGE ATOA MILIONI MBILI KUFIKISHA UMEME KATIKA KIJIJI CHA IVALALILA

Naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la Makete dk Binilithi Satano Mahenge akizingumza na wana nchi wa jimbo wananchi wilayani Makete hivi karibuni (picha na riziki mgaya)

Na Riziki Mgaya

Naibu waziri wa maji na mbuge wa jimbo la Makete DK Binilithi Mahenge ameahidi  kuchangia shilingi milioni mbili katika mradi wa umeme katika kijiji cha Ivalalila wilayani Makete mkoani Njombe.

Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki hii mbele ya wananchi wa Ivalalila akitoa ahadi hiyo  Dk Mahenge alisema  jitihada za wananchi kujitoa na kuanzisha mradi huo wa umeme utokanao na maporomoko ya maji yaliyoko katika  kijiji hicho ni wakuungwa mkono na kila mpenda maendeleo.
 
Pia Mahenge aliwataka wananchi hao kutokata tamaa na maendeleo ya kijiji hicho na kuahidi kuendelea kukisaidia kijiji hicho   kwa kushirikiana  na halimashauri ya wilaya 
“nitawaunga mkono kwakushirikiana na halmashauri ya wilaya kwa kupitia mfuko wa jimbo ili kuwaunga mkono kwa jitihada za maendeleo nimefurahishwa sana na uwajibikaji wenu hii inatia moyo pia natoa rai yangu kwa wananchi wa sehemu nyingine waige mfano huu ili kujikwamua na umasikini” alisema Dk Mahenge.
 
 Awali Dk mahenge alifanya ziara yake katika kijiji cha Ndulamo kilichopo wilayani hapa  na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ambapo walitoa kero zao   mbele ya naibu wa maji ambaye pia ni mbuge wa jimbo hilo huku kero ya maji ikiwagusa sana  wananchi wakijiji hicho na wakalazimika kumueleza Dk Mahenge kilio cha maji  kilichopo kijijini hapo kuwa imekuwa ni moja kati ya vitu vinavyo changia kushuka kwa maendeleo kijijini hapo 
“tunateseka na adha ya maji tunaomba kama mbuge wetu ambaye unasikiliza vilio vya wanachi wako na kwa kuwa ni naibu waziri wa maji tusaidie”walisema wanakijiji hao.
 
Tuesday, December 11, 2012

NYUMBA YA MTUMISHI WA ZAHANATI KUGHARIMU MILIONI 36 MAKETE

Na Eddwin Moshi

Zaidi ya shilingi milioni 36 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa zahanati ya kijiji cha Ivilikinge kilichopo kata ya Isapulano wilayani Makete
Akizungumzia suala hilo ofisini kwake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Mendrad Sanga amesema kwamba ujenzi huo ulianza mwezi Mei mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Februari mwakani
Amesema kwa sasa zahanati hiyo kwa sasa inawahudumu wawili ambapo mmoja kati yao anaishi kwenye nyumba ya kupanga
Katika ujenzi huo serikali imechangia kiasi cha silingi milioni 6 huku milioni 30 ni nguvu za wananchi wa kijiji hicho
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameiomba serikali kuongeza kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi huo kwa kuwa kiasi walichotoa ki kidogo kulingana na ujenzi huo

VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA WILAYANI MAKETE VYATAKIWA KUBUNI MIRADI ENDELEVU YA KUENDESHA VITUO HIVYO

Watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Fema Matamba

Baadhi ya vitu alivyovitoa mkuu wa wilaya

Mkuu wa wilaya ya Makete Mh.Josephine Matiro(katikati) akisikiliza wimbo unaoimbwa na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho(hawapo pichani), kulia kwake ni Askofu wa dayosisi ya kusini magharibi Job Mbwilo na kushoto ni Msimamizi wa kituo Bi Ala Mbwilo

Kituo cha watoto yatima cha FEMA Matamba

Watoto hao wakimuaga mkuu wa wilaya

 Na Edwin Moshi
 
 Vituo vinavyolelea watoto yatima wilayani Makete vimetakiwa kubuni na kuanzisha miradi endelevu itakayosaidia vituo hivyo kuzidi kutoa huduma bila kutegemea wahisani mbalimbali
Imeonekana kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia vituo hivyo kuendelea kuwepo hata kama wafadhili hao watasitisha ufadhili katika vituo hivyo, miradi waliyobuni na kuitekeleza itasaidia kuendesha vituo hivyo
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Fema Matamba kwa lengo la kutoa msaada kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho
Amesema huu sio muda wa kubweteka na kuwategemea wafadhili pekee badala yake ni kuangalia mbele zaidi kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama kilimo ambvyo itasaidia kuleta kipato cha vituo hivyo hasa ukizingatia hivi sasa wahisani wengi wanaanza kujitoa kufadhili masuala mbalimbali
“Sijui kwa nini sisi waafrika tunabweteka sana tunapenda sana misaada na kulalamika kazi hakuna wakati fursa tunazichezea wenyewe tu, sasa sijui tunataka nini, tuamke tutumie fursa tulizo nazo sasa” alisema
Hata hivyo mkuu huyo amepongeza uongozi wa kituo hicho kwa kuwa na moyo wa kusaidia kulea watoto hao yatima ambao mara nyingi jamii imewasahau, na kusema kuwa malipo ya kazi yao yatatolewa na mwenyezi MUNGU
Awali akitoa maelezo kuhusu kituo kwa Mh. Mkuuwa wilaya, msimamizi wa kituo hicho cha Fema Matamba Bi.Ala Mbwilo amesema kituo hicho kinategemea msaada wa wafadhili waliopo nje ya nchi ambao hutoa sh. Milioni 2 kila mwaka fedha ambazo bado hazitoshi kuendesha kituo hicho
Pamoja na hayo amesema ukosefua wa maji nalo ni tatizo lililopo eneo la Matamba ambalo huwalazimu kwenda mtoni kuchota maji ama kwenye bomba za vijiji jirani kwa ajili ya mahitaji ya kituo hicho
“Unajua mkuu watu huwa tunabweteka sana, hatutaki kulima wala kujishughulisha lakini tunapenda misaada tu, sasa misaada ikiisha tunakosa cha kufanya, tunabaki njia panda” alisema Bi. Mbwilo
Naye Askofu wa dayosisi ya kusini magharibi ambayo inamiliki kituo hicho Job Mbwilo ameshukuru kwa ujio huo wa mkuu wa wilaya huku akisema yeye ni kiongozi wa kwanza kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho na kutoa msaada kwa watoto yatima wanaoishi hapo
Amesema wazo alilolitoa la kituo hicho kuwa na miradi endelevu watalifanyia kazi haraka iwezekanavyo kama namna ya kuboresha kituo hicho kwa kuwa jukumu la kuhakikisha watoto yatima popote duniani ni la jamii nzima, hivyo jamii nayo inapaswa kushirikiana kwa pamoja kuwalea watoto hao

Monday, December 3, 2012

MKUU WA WILAYA YA MAKETE AFANYA ZIARA KWENYE MFEREJI WA UMWAGILIAJI KATA YA LUWUMBU

Chanzo cha mfereji huo

Sehemu ya mfereji huo
Matumizi ya mfereji wa umwagiliaji kwenye mashamba ya wakulima katika kata ya Luwumbu wilayani Makete huenda yakaanza mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ujenzi wake kuwa katika hatua za mwisho
Hayo yamesemwa na mkandarasi anayetengeneza mfereji huo wakati akimweleza mkuu wa wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa mfereji huo
Amesema mfereji huo ambao unatakiwa ukamilike ndani ya kipindi cha miezi sita ambapo ni Februari Mwakani, lakini amesema kutokana na hatua ambayo wamefikia sasa ni zaidi ya asilimia 85 na hatua zilizobakia ni chache hivyo ana uhakika wa kukamilisha kazi hiyo kabla ya Februari
Mfereji huo ambao unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa kata hiyo, umejengwa wakati muafaka ambapo mkuu huyo wa wilaya amempongeza mkandarasi huyo ambapo pamoja na mambo mengine amemsisitiza kuhakikisha anaujenga kww kiwango kinachokubalika na serikali, kwa kuwa kumaliza mradi kabla ya wakati uliopangwa mara nyingine ni jambo zuri ila kazi iwe ya kiwango stahili
“Unasikia ndugu mkandarasi, hongera kwa kazi nzuri na hatua uliyofikia lakini ndugu yangu hakikisha hii kazi inakuwa na viwango vinavyotakiwa kwa maana watakapokuja wakaguzi hapa kuikagua ikawa chini ya kiwango sijui utaiambia nini serikali, lakini ukimaliza mapema na ikawa ya kiwango kinachotakiwa kwa kweli ni jambo la heri” alisema Matiro
Wilaya ya Makete ni miongoni mwa wilaya chache hapa nchini zanye vyanzo vingi vya maji ambapo serikali imeanza mchakato wa kuvitumia vyanzo hivyo hivyo kwa uboreshaji wa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambapo imeanza utaratibu wa kutengeneza mifereji ya umwagiliaji