Katika kusherekea sikuu ya mwakampya benki ya NMb tawi la
Makete ilitembea katika hospitali ya
wilaya ya Makete na kuwaliwaza wagonjwa pamoja na kuwapa zawadi za mwaka mpya .
Meneja wa benki hiyo bwana Anyambilile Ambingile alisema
hatua hiyo imekuja baada ya kuona niviziri wakaenda kuwaona wagonjwa ambao wapo
katika hospitali hiyo ili kuwapa moyo wangonjwa pamoja na kuwapa zawadi za
mwaka mpya jambo ambalo litawafanya waongeze matumaini kuweza kupona na baadaye
kiruhusiwa kutoka na wao kama taasisi kuwapa
faraja
Adha Ambingile aliyaomba mashirika taasisi za dini pamoja serikali kuiga mfano huo kwa
kuwatembelea mara kwa mara watu kama hao kwani kwa kufanya hivyo kunaleta
mahusiano mazuri kati ya jamii na taasisi “tunaomba jamii ielewe kuwa suala la
kuwasaidi watu katika jamii ni la kila mtu aliyenacho ndo maana nasema mashika
yaige mfano huu ilikujijengea mazingira mazuri na ushikiano mzura baina ya
taasisi na jamii kwani kwa kufanya hivyo kutasadia jamii iwe na mtazamo mzuri na
kwa taasisi hizo”alisema Ambingile
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa wilaya Michael Guraka
alipongeza kitendo hicho na kuwapongeza benki hiyo kwa kuwakumbuka wagonjwa hao
ambao wamekuwa wakikosa furaha hasa katika msimu huu wa sikuu kwani huwa
wanakosa liwazo kwaupande wake Rehema Mahenge ambaye alilazwa katika wodi ya
wazazi alishukuru kwa uongozi mzima wa benki hiyo kwa kuwakumbuka wagonjwa na
kuwaomba kundlea kufanya hayo zaidi katika siku za usoni na wasishi hapo
No comments:
Post a Comment