Kituo
kilichojengwa kwa ajili ya kulelea watoto yatima kilichopo kijiji cha
Maleutsi wilayani Makete kinakabiliwa na tatizo la kutokuwepo kwa vyoo.
Akizungumza
na wanahabari kituoni hapo msimamizi wa kituo hicho Mchungaji Simoni
Ilomo amesema kuwa tatizo la vyoo limekuwa likikwamisha uzinduzi wa
kituo hicho kilichoanza kujengwa takribani miaka miwili iliyopita chini udhamini wa kanisa la Batheli Morogoro.
Amesema ujenzi wa kituo hicho ulisimamiwa na Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God [T.A.G]
na changamoto kubwa kwa sasa ni kutokuwepo kwa vyoo ambapo ujenzi wa
vyoo vinavyohitajika inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni
kumi na tatu.
Katika hatua nyingine Mch. Ilomo ameongeza kuwa kituo hicho mara baada
ya kuzinduliwa kitaanza kupokea watoto waishio katika mazingira
hatarishi na yatima bila kubagua ukabila wala dini na wanatarajiwa
kujenga chuo cha ufundi kwa ajili ya watakaoshindwa kuendelea na sekondari au kidato cha sita.
Hata
hivyo amesema watoto watakaolelewa pamoja na kusomeshwa na kituo hicho
ni wale walio chini ya umri ya miaka saba pia amewaomba wahisani pamoja
na serikali kusaidia ili kituo kianze kutoa huduma kwa watoto yatima na
wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
No comments:
Post a Comment