chanzo cha maji Ivalalila
Chanzo cha maji cha ivalalila kinacho hudumia wakazi wa Makete kinavyo onekana (Picha na Riziki Mgaya) |
Mtumishi wa mamlaka ya maji akishiriki zoezi la upandaji miti pembezoni mwa chanzo hicho cha maji |
Mamlaka ya maji makete imeanza mikakati ya
kuboresha huduma hiyo ili kuondokana na shida ya upatikanaji wa maji kwa watumiaji
wa huduma hiyo.
Akizungumza na mtandao huu meneja wa Maji Bwana Jornas Ndomba amesema kuwa tayari
wameshanza jitihada za kuongeza kingo za
pembeni katika chanzo kikuu cha maji kilichopo katika kijiji cha Ivalalila kwa Ajili ya kuzuia kupotea kwa maji mengi katika chanzo hicho
Sambamba na hilo pia mamlaka ya maji
imepanda miti aina ya miturunga kuzunguka eneo la chanzo hicho cha maji kwa
ajili ya kusaidia uhifadhi wa kisima hicho kutoka na miti hiyo kuto tumia maji mengi.
Katika hatua
nyingine bwana Ndomba amewaomba wakazi wa Ivalalila kukitunza chanzo hicho kwa
kutoendeleza shughuli za kibinadamu katika chanzo hicho kwani kuna baadhi ya
watu wamekuwa na tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo
ufugaji na upandaji wa miti bila kuzingatia sheria za uhifadhi wa vyanzo vya maji
No comments:
Post a Comment