Na Hadija Sanga
Zaidi
ya shilingi milioni 80 zimetumika hadi sasa katika ujenzi wa Zahanati
ya kijiji cha Ivalalila wilayani Makete, ujenzi ambao bado unaendelea
Hayo
yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Ivalalila Bw. Fidelis Sanga
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na
ujenzi huo ambao ulianza tangu mwaka 2010 kwa nguvu za wananchi kwa
kushirikiana na serikali
Amesema mpaka sasa ujenzi huo unaendelea vizuri na umefikia hatua ya upauaji wa jengo hilo
huku akisisitiza kuwa mradi huo umepokelewa kwa mikono miwili na
wananchi wa kijiji hicho na ndio maana ujenzi huo umefikia hatua nzuri
Bw.
Sanga amezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kwa sasa
katika ujenzi huo kuwa ni pamoja na uhaba wa fedha za kuendelea na mradi
huo pamoja na uchache wa wananchi wanaokuja kushiriki katika ujenzi huo
Aidha
ametoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali kujumuika pamoja kushiriki
ujenzi wa zahanati hiyo kwa namna moja ama nyingine pamoja na wananchi
kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shughuli za ujenzi huo pale
wanapohitajika kufanya hivyo
Habari Kwa msaada wa Eddymoblaze.blogspot.com
No comments:
Post a Comment