Social Icons

Saturday, November 24, 2012

PIKI PIKI ZA WAGONJWA ZAENDELEA KUOZA JK HAJUI HILO?

PIKI PIKI HIZI ZIPO HOSPITALI YA WILAYA MAKETE HAZIFANYI KAZI

WANYAMA KUZINDUA DARAJA DESEMBA MOSI MWAKA HUU

Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara na Daraja la luwumbu kata ya luwumbu wilaya ya makete iliyojengwa kwa msaada wa mfanya biashara maalufu jijini dar es salaam Bwana Wanyama na wananchi kuanza kulitumia uzinduzi wadaraja hilo unatarajiwa kufanyika tarehe mosi desemba mwaka huu

akizungumza na mtandao huu Mfanya biashara huyo amesema uzinduzi huo utafanyika siku ya juma mosi na wanatarajia kuwaaalika watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa na wa serikali na wananchi wote wa kata yaluwumbu na maeneo jirani

akizungumzi uamuzi wake wa kujenga daraja hilo Bwana Wanyama amesema kijiji cha luwumbu ndiko aliko zaliwa na tangu utoto wake amekuwa akiona wazazi wake wakipata shida ya kuvuka katika daraja dogo la miti lililokuwepo katika mto huo hivyo ameamua kuonyesha mchango wake kwa jamii ya wana luwumbu

aidha amewataka wafanyabiashara wenzake na watu wenye mafanikio kusaidia kule walikotoka ili kuwapunguzia matatizo ndugu zao wa kipato cha chini na wale wasio na uwezo kama wao

hii itakuwa cni mara ya kwanza kwa mfanya biashara kuamua kusimamia ujenzi mkubwa kama huo ulio gharimu pesa nyingi kama huo kwani daraja hilo pamoja na barabara vimegharimu zaidi ya shilingi milioni sabini

Wednesday, November 14, 2012

UJENZI ZAHANATI YA IVALALILA WASUASUA



Na Hadija Sanga
Zaidi ya shilingi milioni 80 zimetumika hadi sasa katika ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Ivalalila wilayani Makete, ujenzi ambao bado unaendelea
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Ivalalila Bw. Fidelis Sanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na ujenzi huo ambao ulianza tangu mwaka 2010 kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali
Amesema mpaka sasa ujenzi huo unaendelea vizuri na umefikia hatua ya upauaji wa jengo hilo huku akisisitiza kuwa mradi huo umepokelewa kwa mikono miwili na wananchi wa kijiji hicho na ndio maana ujenzi huo umefikia hatua nzuri
Bw. Sanga amezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kwa sasa katika ujenzi huo kuwa ni pamoja na uhaba wa fedha za kuendelea na mradi huo pamoja na uchache wa wananchi wanaokuja kushiriki katika ujenzi huo
Aidha ametoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali kujumuika pamoja kushiriki ujenzi wa zahanati hiyo kwa namna moja ama nyingine pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shughuli za ujenzi huo pale wanapohitajika kufanya hivyo
 
Habari Kwa msaada wa Eddymoblaze.blogspot.com

MAMLAKA YA MAJI MAKETE YA HIMIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI


 chanzo cha maji Ivalalila
Chanzo cha maji cha ivalalila kinacho hudumia wakazi wa Makete kinavyo onekana (Picha na Riziki Mgaya)

Mtumishi wa mamlaka ya maji akishiriki zoezi la upandaji miti pembezoni mwa chanzo hicho cha maji
Mamlaka ya maji makete imeanza mikakati ya kuboresha huduma hiyo ili kuondokana na shida ya upatikanaji wa maji kwa watumiaji wa huduma hiyo.
Akizungumza na mtandao huu meneja wa Maji Bwana Jornas Ndomba amesema kuwa tayari wameshanza  jitihada za kuongeza kingo za pembeni katika chanzo kikuu cha maji kilichopo katika kijiji cha Ivalalila kwa Ajili ya kuzuia kupotea kwa maji mengi katika chanzo hicho
 
 
Sambamba na hilo pia mamlaka ya maji imepanda miti aina ya miturunga kuzunguka eneo la chanzo hicho cha maji kwa ajili ya kusaidia uhifadhi wa kisima hicho kutoka na miti hiyo kuto tumia maji mengi.
  
Katika hatua nyingine bwana Ndomba amewaomba wakazi wa Ivalalila kukitunza chanzo hicho kwa kutoendeleza shughuli za kibinadamu katika chanzo hicho kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo ufugaji na upandaji wa miti bila kuzingatia sheria za uhifadhi wa vyanzo vya maji

Saturday, November 10, 2012

BARABARA YA LAMI MAKETE YA ENDELEA KUSOGEA

Ujenzi ukiendelea katika barabara ya Njombe Makete kwa kiwango cha lami (picha zote na Riziki Mgaya)
 
 
 
Wananchi waipongeza serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha inaboresha miundombinunuya barabara wilayani Makete kwa kuongeza kilomita moja ya barabara ya lami baada ya kukamilika kipande cha awali cha Mang'oto Usungilo

Wakizungumza na mtandao huu Wananchi wa kijiji cha Usungilo kata ya Tandala wamesema kukamilika kwa kipande hicho kitasidia kwa kiwango kikubwa kupunguza adha waliyokuwa wakiipata watumiaji wa barabara hiyo hususani katika kipindi cha masika

wamesema eneo hilo lilikuwa likisumbua sana kutokana na udongo wake kuwa wamfinyanzi jambo lilokuwa likichangia kwa magari kukwama kutokana na kuchimbika sana

aidha wameiomba serikalio kumsimamia mkandarasi canopies international kufanya kazihiyo kwa wakati ili kuepusha adha inayoweza kujitokeza ya magari kukwama kipindi hichi ambacho mvua zimeanza kunyesha


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Thursday, November 8, 2012

KUTOKUWEPO KWA CHOO KWA KWAMISHA UZINDUZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA


Kituo kilichojengwa kwa ajili ya kulelea watoto yatima kilichopo kijiji cha Maleutsi wilayani Makete kinakabiliwa na tatizo la kutokuwepo kwa vyoo.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo msimamizi wa kituo hicho Mchungaji Simoni Ilomo amesema kuwa tatizo la vyoo limekuwa likikwamisha uzinduzi wa kituo hicho kilichoanza  kujengwa takribani miaka miwili iliyopita chini udhamini wa kanisa la Batheli Morogoro.
Amesema ujenzi wa kituo hicho ulisimamiwa na Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God  [T.A.G] na changamoto kubwa kwa sasa ni kutokuwepo kwa vyoo ambapo ujenzi wa vyoo vinavyohitajika inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu.
Katika hatua nyingine Mch. Ilomo ameongeza kuwa kituo hicho mara  baada ya kuzinduliwa kitaanza kupokea watoto waishio katika mazingira hatarishi na yatima bila kubagua ukabila wala dini na wanatarajiwa kujenga chuo cha ufundi kwa ajili ya watakaoshindwa kuendelea  na sekondari au kidato cha sita.
Hata hivyo amesema watoto watakaolelewa pamoja na kusomeshwa na kituo hicho ni wale walio chini ya umri ya miaka saba pia amewaomba wahisani pamoja na serikali kusaidia ili kituo kianze kutoa huduma kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Wednesday, November 7, 2012

MISAADA YA WATOTO YATIMA LAZIMA IWANUFAISHE WATOTO WENYEWE


watoto yatima wakiwa na magodoro yao

Wafanyakazi wa shirika la ELCT Makete - Pamoja Tuwalee program

Mratibu wa pamoja tuwalee MCh. Ezekiel Sanga (katikati) akiwa na wafanyakazi wenzake


Mgeni rasmi Mh. Daniel Okoka akimgawia mtoto yatima viatu


Mh. Daniel Okoka akitoa hotuba yake
Serikali imewataka viongozi wa kijiji cha Lumage kata ya Iniho wilayani Makete kuhakikisha inafuatilia na kujua kama nyumba ni hitaji muhimu la watoto yatima waliopo kwenye kijiji hicho pamoja na walezi kutowanyang’anya misaada wanayopewa watoto hao na kuifanya yao
Hayo yamesemwa na Mgeni rasmi katika hafla ya kugawa magodoro tisa kwa watoto yatima waliopo kijijini hapo yaliyotolewa na kikundi cha kuweka na kukopa kijijini hapo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka
Mh. Okoka amesema wakati mwingine ni vigumu kuona mtoto yatima hana hata ndugu mmoja hivyo anakosa mahali pa kukaa, ila anachoamini ni kwamba watoto hao wana ndugu lakini wengi wao wanawatesa watoto hao
“Ndugu zangu mimi sidhani kama kuna mtoto hata mmoja ambaye hana ndugu, inawezekana yupo lakini sina uhakika, ndugu walioachiwa watoto hawa wanapaswa kuwatunza kwa upendo ili wasitoroke majumbani” alisema Okoka na kuongeza “ leo tumewapa magodoro haya, ni kwa ajili ya watoto yatima sasa walezi masije mkawanyang’anya watoto na mkayafanya ya kwenu kwa sababu hiyo ndiyo tabia ya watu wengi, mnamnyang’anya mtoto godoro yeye anaendelea kulala chini, watoto mkiona mmefanyiwa hivyo toa taarifa kwa uongozi wa kijiji haraka”
Akizungumzia ushirikiano uliofanywa na Mratibu wa program ya Pamoja Tuwalee wilayani hapa Mch. Ezekiel Sanga, mh Okoka amesema serikali inatambua msaada unaotolewa na mashirika ya dini kuleta maendeleo hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee zaidi na zaidi
Pia amesema wazo la program hiyo kuanzisha vikundi vya SILK ni muhimu na lenye kuinua kipato cha wananchi wake huku akisema uongozi wa wilaya ya Makete upo kwenye mchakato wa kuanzisha Benki ya wananchi wa Makete ambayo itakuwa ikishirikiana na vikundi hivyo vya SILK kuinua uchumi wa wanamakete
“Nawahakikishieni sisi kama wilaya tumeshakutana na wanamakete waliopo Dar es Salaam ambao wanafanya kazi kwenye benki mbalimbali na hata kwenye nafasi zingine, wamekubali na wanalishughulikia na muda si mrefu benki hiyo itaanza” alisema Okoka
Katika kukiunga mkono kikundi hicho mgeni rasmi Mh. Okoka alikipa shilingi 50,000/= pamoja na ada ya kujiunga kama mwanachama wa kikundi hicho ya shilingi 50,000/=, viatu kwa watoto hao yatima pamoja na kuahidi kutoa shuka na blanketi kwa kila mtoto aliyepewa godoro
Akizungumza hatua hiyo mratibu wa Program ya Pamoja Tuwalee inayofanya shughuli hiyo kupitia shirika la ELCT Makete Mch. Ezekiel Sanga amesema jukumu la kuwalea watoto yatima ni la kila mmoja hivyo kila mmoja wetu anapaswa kuwasaidia kwa chochote kile ili kuwapa faraja kutokana na kupoteza wazazi wao
Katika kuliunga mkono hilo Mchungaji huyo alianzisha harambee Fulani ya fedha kwa ajili ya yatima katika kijiji hicho ambapo jumla ya fedha taslim tsh. 153,600/- zilichangwa kwa ajili ya watoto yatima wengine kununuliwa mahitaji mbalimbali