Social Icons

Saturday, November 3, 2012

MAFUNZO YA MGAMBO YA FUNGWA RASMI LEO



 Mgambo wenyewe
 Mshauri wa mgambo wilaya ya Makete Bw. Mfuse
Mkuu wawilaya ya makete Bi Josephin Matilo akifunga mafunzo hayo
 Mgambo akisoma risala kwa mgeni rasmi


 Mkuu wa wilaya akigawa vitambulisho kwa mgambo
 Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro(wa pili kulia) akicheza muziki na mgambo hao

Vijana mia moja na ishirini na mbili wahitimu mafunzo ya mgambo katika kata za Iwawa na Tandala huku wengine sabini na nane wakishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu za ugonjwa na wengine wakikimbia mafunzo hayo

Akifunga mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Makete Bi Josephin Matiro amewapongeza wa hitimu hao kwa uvumilivu na kujituma kwao hadi hitimu mafunzo hayo yaliyodumu kwa miezi minne

Amesema mafunzo hayo yanalengo la kuisaidia jamii kulinda mali zao lakini pia yana wasaidia wahitimu mbinu mbali mbali za kupambana na uhalifu na kupata mbinu za  kujitegemea  kimaendeleo

Aidha Bi Josephin ameahidi kuanzisha kambi ya vijana itakayo jihusisha na kilimo cha kisasa kilimo kitakacho wasaidia kuondokana na umaskini unao wakabili watanzania wengi lakini pia mpango huo utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwao

Amesema vijana wengi wamekuwa wakilalamikia swala la ukosefu wa ajira wakati kuna fursa nyingi za kuweza kuwasaidia kuji kwamua kimaisha moja wapo ikiwa ni kutumia ardi iliyopo kwa matumizi ya kilimo

Amewataka vijana hao kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine walio shindwa kuendelea na mafunzo hayo kwa kufanya mambo yasiyo kinyume na maadili na sheri za nchi huku wakichangamkia fursa mbalimbali zinazo jitokeza katika wilaya yao

Kwa upande wao wahitmu wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kupambana na uharifu kuzuia mianya ya Rushwa na vilevile wamefundishwa mbinu za kupambana na umaskini kutokana na mafunzo ya kujitegemea waliyopewa

Aidha wameiomba serikali kuongeza posho kwa wa kufunzi wanao jitolea kwani wamefanya kazi kubwa kwa mda miezi minne lakini malipo wanayopewa ni kidogo mno na kutaka wenzao walioshindwa kumaliza mafunzo hayo kwa uvivu wachukuliwe hatua za kisheria ili kuyafanya mafunzo hayo yaonekane ya maana

Kwa upande wake Diwani Wakata ya Tandala Mheshimiwa Agnatio Mtawa amesema kambi ya vijana itaundwa kuonyesha kuwea wanaunga mkono harakati za mkuu wa wilaya ya makete Bi Josephin Matiro za kuondoa umaskini hususani kwa vijana

Aidha amewapongeza wahitimu hao na kusema kuwa atashirikiana nao kwa kila jambo watakalo hitaji kutoka kwake ili kuhakikisha raia wanakuwa salam pamoja na malizao lakini pia ili kuondoa dhana ya kwamba vijana hao walikuwa wakipoteza muda katika mafunzo hayo.   

No comments:

Post a Comment