Social Icons

Thursday, November 1, 2012

WANYAMA AONYESHA UZALENDO KWA WANAMAKETE KWA VITENDO


Wananchi wa kijiji cha luhumbu kata yaluwumbu wilaya ya makete  wamemshukuru mfanya biashara maalufu jijini Dar es salaam bwana wanyama kwa msaada wa ujenzi wa daraja linalo unganisha vitongoji viwili
Wamesema kwa kipindi kirefu walikuwa wakipata shida kutokana na ubovu wa daraja hilo hivyo kupatikana kwa daraja hilo kwao ni jambo ambalo hawakutarajia kama lingekuja tokea kwani wameishi kwa zaidi ya miaka hamsini bila kupata daraja kama hilo
Aidha wame waomba wanamakete wenye uwezo wanaoishindani na nje ya makete kuiga mfano wa bwana wanyama aliyetumia uwezo wake kuwasaidia wananchi wa hali ya chni kama wao jambo amblo ni lakumpongeza
 Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni hamsini kwaniaba ya  Wanyama bwana Denis Sanga amesema mfadhili ni mzaliwa wa kijiji hicho na ameguswa na hali mbaya ya miundombinu ndio sababu I,liyompelekea kujitolea kujenga barabara hiyo
Aidha amewataka wananchi kuilinda na kitunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa mdarefu zaidi na iweyenye faida kwa kizazi cha sasa na cha baadae huku akitoa wito kwa serikali kusaidia wananchi katika kufikisha huduma zingine muhimu kama maji na afya.

No comments:

Post a Comment