![]() |
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa choo cha soko |
![]() |
Vyoo vilivyo jengwa na halmashauri vilivyo jaa |
![]() |
Kibanda cha kukusanyia mapato ya halmashauri kwa wanao kwenda kupata huduma ya choo |
![]() |
soko la vyakula linavyo onekana |
Wafanyabiashara wa soko la
makete waendelea na ujenzi wa choo cha soko baada ya ongozi wa halmashauri ya
wilaya ya makete kukataa kujenga choo hicho kilicho ndani ya eneo la
halmashauri
Akizungumza na mtandao huu
mwenyekiti wa soko bwana Hosia Mpandila amesema baada ya halmashauri kukataa
kusaidia ujenzi huo kwa madai ya kutokuwa na fedha waliamua kuanza
kuchangishana fedha za ujenzi huo ambapo kila mfanya biashara alichangia kiasi
cha shilingi elfu kumi
Amesema kweasasa wamemaliza
ujenzi wa shimo na wameanza ujenzi wa vyumba ambao unaendelea vizuri na
kuwataka wafanya biashara ambao hawajakamilisha michango yao kuiwasilisha kwa wakati kwa viongozi wa
kamati ya ujenzi wa choo hicho
Amesema awali choo kilikuwa
kinajengwa na halmashauri ya wilaya ya makete lakini wameshangazwa na kitendo
cha halmashauri kukataa kuwasaidia ujenzi huo huku wakitishiwa kuhamishiwa
katika soko la ngiu kama hawata jenga choo
hicho
Soko lamakete mjini lina
wafanya biashara wapatao miambili na watu wanoingia kuhudumiwa hapo wanakadiliwa
kuwa ni mianne kwa siku jambo ambalo ni hatari kwa afya zao kama
pasipo kuwa na choo cha uhakika.
No comments:
Post a Comment