Zaidi ya shilingi milioni 36 zinatarajiwa kutumika katika
ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa zahanati ya kijiji cha Ivilikinge kilichopo
kata ya Isapulano wilayani Makete
Akizungumzia suala hilo
ofisini kwake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Mendrad Sanga amesema kwamba
ujenzi huo ulianza mwezi Mei mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Februari
mwakani
Amesema kwa sasa zahanati hiyo kwa sasa inawahudumu wawili
ambapo mmoja kati yao
anaishi kwenye nyumba ya kupanga
Katika ujenzi huo serikali imechangia kiasi cha silingi
milioni 6 huku milioni 30 ni nguvu za wananchi wa kijiji hicho
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameiomba serikali
kuongeza kiasi cha fedha kwa ajili ya ujenzi huo kwa kuwa kiasi walichotoa ki
kidogo kulingana na ujenzi huo
No comments:
Post a Comment