
Chanzo cha mfereji huo
Sehemu ya mfereji huo
Matumizi
ya mfereji wa umwagiliaji kwenye mashamba ya wakulima katika kata ya Luwumbu
wilayani Makete huenda yakaanza mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ujenzi wake
kuwa katika hatua za mwisho
Hayo
yamesemwa na mkandarasi anayetengeneza mfereji huo wakati akimweleza mkuu wa
wilaya ya Makete mh. Josephine Matiro alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa
mfereji huo
Amesema
mfereji huo ambao unatakiwa ukamilike ndani ya kipindi cha miezi sita ambapo ni
Februari Mwakani, lakini amesema kutokana na hatua ambayo wamefikia sasa ni
zaidi ya asilimia 85 na hatua zilizobakia ni chache hivyo ana uhakika wa
kukamilisha kazi hiyo kabla ya Februari
Mfereji
huo ambao unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa kata hiyo, umejengwa wakati
muafaka ambapo mkuu huyo wa wilaya amempongeza mkandarasi huyo ambapo pamoja na
mambo mengine amemsisitiza kuhakikisha anaujenga kww kiwango kinachokubalika na
serikali, kwa kuwa kumaliza mradi kabla ya wakati uliopangwa mara nyingine ni
jambo zuri ila kazi iwe ya kiwango stahili
“Unasikia
ndugu mkandarasi, hongera kwa kazi nzuri na hatua uliyofikia lakini ndugu yangu
hakikisha hii kazi inakuwa na viwango vinavyotakiwa kwa maana watakapokuja
wakaguzi hapa kuikagua ikawa chini ya kiwango sijui utaiambia nini serikali,
lakini ukimaliza mapema na ikawa ya kiwango kinachotakiwa kwa kweli ni jambo la
heri” alisema Matiro
Wilaya
ya Makete ni miongoni mwa wilaya chache hapa nchini zanye vyanzo vingi vya maji
ambapo serikali imeanza mchakato wa kuvitumia vyanzo hivyo hivyo kwa uboreshaji
wa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambapo imeanza utaratibu wa kutengeneza
mifereji ya umwagiliaji
No comments:
Post a Comment