Social Icons

Monday, December 17, 2012

MBUNGE ATOA MILIONI MBILI KUFIKISHA UMEME KATIKA KIJIJI CHA IVALALILA



Naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la Makete dk Binilithi Satano Mahenge akizingumza na wana nchi wa jimbo wananchi wilayani Makete hivi karibuni (picha na riziki mgaya)

Na Riziki Mgaya


Naibu waziri wa maji na mbuge wa jimbo la Makete DK Binilithi Mahenge ameahidi  kuchangia shilingi milioni mbili katika mradi wa umeme katika kijiji cha Ivalalila wilayani Makete mkoani Njombe.

Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki hii mbele ya wananchi wa Ivalalila akitoa ahadi hiyo  Dk Mahenge alisema  jitihada za wananchi kujitoa na kuanzisha mradi huo wa umeme utokanao na maporomoko ya maji yaliyoko katika  kijiji hicho ni wakuungwa mkono na kila mpenda maendeleo.
 
Pia Mahenge aliwataka wananchi hao kutokata tamaa na maendeleo ya kijiji hicho na kuahidi kuendelea kukisaidia kijiji hicho   kwa kushirikiana  na halimashauri ya wilaya 
“nitawaunga mkono kwakushirikiana na halmashauri ya wilaya kwa kupitia mfuko wa jimbo ili kuwaunga mkono kwa jitihada za maendeleo nimefurahishwa sana na uwajibikaji wenu hii inatia moyo pia natoa rai yangu kwa wananchi wa sehemu nyingine waige mfano huu ili kujikwamua na umasikini” alisema Dk Mahenge.
 
 Awali Dk mahenge alifanya ziara yake katika kijiji cha Ndulamo kilichopo wilayani hapa  na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ambapo walitoa kero zao   mbele ya naibu wa maji ambaye pia ni mbuge wa jimbo hilo huku kero ya maji ikiwagusa sana  wananchi wakijiji hicho na wakalazimika kumueleza Dk Mahenge kilio cha maji  kilichopo kijijini hapo kuwa imekuwa ni moja kati ya vitu vinavyo changia kushuka kwa maendeleo kijijini hapo 
“tunateseka na adha ya maji tunaomba kama mbuge wetu ambaye unasikiliza vilio vya wanachi wako na kwa kuwa ni naibu waziri wa maji tusaidie”walisema wanakijiji hao.
 

No comments:

Post a Comment