Jumla ya mbuzi
112 wamegawiwa kwa baadhi ya vikundi vya shirika la MASUPHA wilayani
Makete kwa lengo la kuboresha lishe na kuinua uchumi wa vikundi hivyo
Akizungumza na
mwanahabari wetu wakati wa ugawaji mbuzi hao, mkurugenzi wa shirikala
MASUPHA Bi Aida Chengula amesema shirika hilo lilijadili kwa pamoja na
wanavikundi hao ambapo wao wenyewe walipendekeza kuwa wanahitaji mbuzi
wa kisasa wa maziwa na ndiyo maana wamewapatia mbuzi hao
Bi Chengula
amesema baadhi ya vikundi hivyo vinajumuisha walemavu na wenye virusi
vya UKIMWI ambao mara nyingi husahaulika hivyo mbuzi hao watainua uchumi
wao na kuongeza kuwa wamewapata mbuzi hao kwa ufadhili wa RFE
Naye afisa
ufuatiliaji na tathmini kutoka RFE Bw. Julius Mkandara amesema mbuzi hao
wa kisasa ni faraja kwa wanavikundi hao na ni namna mojawapo ya
kuheshimu mawazo yao
Amesema mbuzi hao watakapozaliana watapata maziwa ya kunywa na kuuza na mbuzi wa kuuza kama njia mojawapo ya kujipatia kipato pamoja na mbolea kwa ajili ya bustani za mbogamboga
Mmoja wa
wanakikundi kutoka kata ya Isapulano aliyejitambulisha kwa jina la
Monica Mahenge amesema mbuzi hao watamsaidia kuendesha familia ikiwemo
kusomesha watoto
Shirika la MASUPHA limekuwa likisaidia kuvipa vikundi vyake mikopo yenye riba nafuu pamoja na misaada mbalimbali ikiwemo mifugo kama mbuzi kwa lengo la kuvikwamua kiuchumi
No comments:
Post a Comment