Social Icons

Saturday, October 27, 2012

MADIWANI MAKETE WAFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA WA BARABARA ZA MITAA


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka



Waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete wamefanya ukaguzi wa barabara katika baadhi ya maeno katika kata ya Iwawa ambazo zilifanyiwa ukarabati hivi karibuni
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza ukaguzi huo wa kushtukiza mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete mh. Daniel Okoka ambaye aliongozana na madiwani wenzake amesema wameweza kukagua miundombinu ya barabara kuelekea halmashauri ya Makete (Bomani), Tanesco na nyinginezo za mitaa mbalimbali ya kata ya Iwawa

Mh. Okoka amesema kuwa anawaomba wananchi kutokuharibu miundombinu kwa kutupa takataka kwenye mifereji ya maji kandokando mwa barabara pamoja na kwenye makalavati kwani vinaharibu barabara
Hata hivyo Mh. Okoka amewaasa wananchi kutambua kuwa wao ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kutunza barabara hizo na pia ameongeza kuwa kabla ya kuanza kwa matengenezo ya barabara wananchi watatakiwa kutoa maoni juu ya ujenzi wa barabara
Ukaguzi huo umefanywa kufuatia barabara hizo kujengwa chini ya kiwango, hali iliyopelekewa kulaumiwa na wananchi, lakini Mh. Okoka hakutaka kuliweka hilo wazi na badala yake amesema wameamua kufanya hivyo ili kuweza kulijadili katika vikao vyao vya ndani na taarifa itatolewa baadaye
Amesema badabara hizo zitatakiwa kufanyiwa marekebisho pamoja na kuzibuliwa kwa mitaro iliyojiziba kwa vumbi jingi pamoja na kifusi kizuri kwenye barabara hizo ili kuepuka vumbi lisilo na ulazima

 

No comments:

Post a Comment