Social Icons

Saturday, October 27, 2012

WANAMAKETE WASHAURIWA KUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI



Wananchi wilayani Makete wameshauriwa kutumia huduma za kibenki kutokana na elimu wanayoipata juu ya huduma hizo

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Iwawa Meneja wa benki ya NMB tawi la Makete Bw. Peter kinyosa amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma ya kuweka na kutoa fedha, mikopo pamoja na kufungua akaunti kwa wateja wapya

Amesema matumizi ya huduma za kibenki hayana usumbufu hivyo ni wakati muafaka kwa wananchi kuhifadhi fedha zao benki kwani ni sehemu salama na yenye uhakika zaidi

Pia meneja huyo ametoa wito kwa wateja wa benki yake kuhifadhi taarifa zao za siri za kibenki ili kuepukana na wimbi la matapeli ambao wanaweza kuwaibia fedha zao

Naye afisa mikopo wa NMB Makete Bw. Rodrick Mollel amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia mikopo wanayoipata kufanyia shughuli za kimaendeleo ili kuinua kipato chao pamoja na kunufaika na mikopo hiyo

Ameelezea changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kutoa mikopo kuwa ni usumbufu kutoka kwa wateja wakati wa kurejesha fedha walizokopa pamoja na kutokuwa na viambatanisho muhimu vinavyohitajika kabla ya kupewa mkopo

No comments:

Post a Comment