Social Icons

Thursday, November 1, 2012

PAMOJA TUWALEE WATOA KUKU KUSAIDIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KIJIJI CHA IWAWA

Watoto watano wanaoishi katika mazingira hatarishi katikakijiji cha iwawa kata ya iwawa wilayani makete wamekabidhiwa kuku kumi wa kwa ajiri ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji huku wengine wakipatiwa simbilisi na kumi nanane wakikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vyeti hivyo wazazi na walezi wa watoto hao afis ustawi wa jamii na lishe wa mradi wa pamoja tuwalee unao simamiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Dayosisi ya kusini kati Bi Atuwene Mwike amesema lengo la kuwakabidhi watoto hao mradi wa kuku ni kuwasaidia kupunguza ukali wa ugumu wa  maisha unao wakabili
Amesema kwa kipindi kirefu watotio wanao ishi katika mazingira magumu wamekuwa wakipatiwa misaada ambayo siyo endelevu na pindi mashirika yanayotoa misaada yanpo maliza miradi yao watoto wamejikuta katika m agumu zaidii hivyo kwa kuwaanzishia miradi kama hiyo watoto watakuwa katika mazingia mazuri ya kujitegemea wenyewe


Akizungumzia swala la vyeti vya kuzaliwa bi mwike amesema wamegun dua kuwa watoto wengi wanao ishi kwenye mazingira hatarishi hawana vyeti vya kuzaliwa jambo ambalo lini haki yao ya msingi kuwanavyo hivyo wao wamekuwa wakiwasaidia watoto kupata vyeti hivyo


Kwa upande wake mwenyekiti wa mvc kijiji cha iwawa bwana Dange Sanga amesema kukabidhiwa vyeti na kuku kwa watoto hao ni msaada mkubwa kwa watoto na walezi wao wanaoishi katika mazingira hatarishi kwani wengi wao wamekuwa hawana miradi yoyote katika kaya zao


Aidha amewasisitiza walezi wa watotohao jkujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kukuza vipato vya kaya zao na waweze kuwaendeleza watoto kitaalunma na kuondokana na umaskini unao wakabili.


Katika mkutano huo wazazi na walezi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wamejiorodhesha kwa ajihri ya kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopeshana ambapo faida itakayo patikana kutokana na vikundi hivyo itatumika katika kuwanunulia watoto vifaa vya shule na kuwatatulia matatizo yanayo wakabili.

No comments:

Post a Comment