Social Icons

Wednesday, November 14, 2012

UJENZI ZAHANATI YA IVALALILA WASUASUA



Na Hadija Sanga
Zaidi ya shilingi milioni 80 zimetumika hadi sasa katika ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Ivalalila wilayani Makete, ujenzi ambao bado unaendelea
Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Ivalalila Bw. Fidelis Sanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na ujenzi huo ambao ulianza tangu mwaka 2010 kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali
Amesema mpaka sasa ujenzi huo unaendelea vizuri na umefikia hatua ya upauaji wa jengo hilo huku akisisitiza kuwa mradi huo umepokelewa kwa mikono miwili na wananchi wa kijiji hicho na ndio maana ujenzi huo umefikia hatua nzuri
Bw. Sanga amezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kwa sasa katika ujenzi huo kuwa ni pamoja na uhaba wa fedha za kuendelea na mradi huo pamoja na uchache wa wananchi wanaokuja kushiriki katika ujenzi huo
Aidha ametoa wito kwa serikali na wadau mbalimbali kujumuika pamoja kushiriki ujenzi wa zahanati hiyo kwa namna moja ama nyingine pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye shughuli za ujenzi huo pale wanapohitajika kufanya hivyo
 
Habari Kwa msaada wa Eddymoblaze.blogspot.com

No comments:

Post a Comment